Kwa mujibu wa Idara ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, Ofisi ya Ayatullah Sayyid Ali Sistani nchini Lebanon, kupitia taarifa iliyotoa, imetangaza kuanzishwa mpango mpya wa kibinadamu wa kutoa msaada wa kifedha kwa yatima waliotokana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi hiyo.
Mpango huo unalenga kuwasaidia yatima ambao hawako chini ya uangalizi wa taasisi yoyote au jumuiya ya hisani, kwa kuwapatia msaada wa kifedha wa kila mwezi.
Lengo kuu la mpango huu ni kupunguza maumivu na mateso wanayopitia yatima walioathiriwa na vita nchini Lebanon.
Maoni yako